Abstract:
Tasnifu hii inajikita katika uchunguzi wa fani katika riwaya mbili za Said Ahmed Mohamed. Riwaya zenyewe ni Qggig Mti Mkavu (1980) na Kiza Katika Nuru (1988). Tunaoyesha kuwa Mohamed, kama baadhi ya watunzi wengine wa kazi za ubunifu, ameathiriwa na miktadha ya kijamii na kijiografia katika uchujaji na uchotaji wa mbinu za kifani. Aidha. tunabainisha kuwa, ili kazi ya ubunifu idhihirishe utimilifu wa kifasihi, ni sharti vipengele vya fani vionyeshe muwala au muumano. Katika mkabala huu, tumeonyesha jinsi riwaya ya Dunia Mti Mkavu ilivyokosa muwala ikilinganishwa na riwaya ya Kiza katika Nuru, hivyo umaarufu wake kutopata uhai. Vilevile, tunaonyesha kuwa vipengele vya fani na maudhui vinachukua uzito sawa katika kazi ya kubuni——hakuna kipengele kinachojitokeza kuwa muhimu zaidi ya kingine. Ili kufanikisha maazimio yetu, tumeshughulikia vipengele vya ploti, wahusika na uhusika, mandhari na mtindo. Tasnifu hii imegawanywa katika sura sita kuu. Sura ya kwanza, hasa, ni utangulizi. Sura hii inafafanua mada ya tasnifu yetu, madhumuni ya utafiti, umuhimu wa mada tunayoshughulikia. nadharia zinazotuongoza katika utafiti huu, upeo wake, tafiti za awali kuhusiana na mada hii pamoja na mbinu za kitafiti tunazozitumia ili kufanikisha utafiti wetu. Sura ya pili inatoa, kwa muhtasari, maisha ya Said Ahmad Mohammed ni muhimu katika sura ya nne tunapochunguza athari za mazingira zinazomwathiri Mohamed katika uchujaji na uchotaji wa mbinu za kifani. Ni katika sura hii ambapo tumevijadili vipengeie muhimu vya fani ambavyo ndivyo nguzo ya kazi ya kubuni. Kwa jumla, sura hii ndiyo msingi wa yanayofuata katika sura ya tatu. Sura ya tatu inajihusisha na uhakiki wa vipengele vya fani katika riwaya tunazozifanyia utafiti. Sura hii ndiyn nguzo kuu, na inajenga msingi wa yale yanayojadiliwa katika sura za nne na tano. Ni katika sure hii, ambapo tumekadiria tafiti za awali kuhusiana na fani. Vipengele vya ploti. wahusika, mandhari na mtindo vimejadiliwa kwa marefu na mapana. Sura za nne na tano ndizo kiini cha tasnifu nzima. Tunaonyesha katika sura ya nne jinsi Said Ahmed Mohamed anavyoathiriwa na miktadha ya kijamii na kijiografia. Sura ya tano inaonyesha bayana jinsi muwala wa vipengele vya fani katika riwaya ya Dunia Mti Mkavu unavyofifia, hivyo kuikosesha ukamilifu na utimilifu wa kifasihi. Pia. inaonyesha Mohamed amejenga vipengele vya fani huku vikidhihirisha muwala katika Kiza Katika Nuru, jambo ambalo linaifanya kudhihirisha dtimilifu wa kifasihi. Halikadhalika, ni katika sura hii ambapo tunaonyesha usawa wa fani na maudhui baada ya kuhakiki vipengele vya fani na kuchunguza muwala wake. Hatimaye, katika sura ya sita, ambayo ndiyo ya mwisho, tunatoa muhtasari wa tasnifu nzima na matokeo ya utafiti wetu. Pia, sura hii inaangaza matatizo tuliyokumbana nayo katika utafiti huu. Baadhi ya mapendekezo zaidi ya utafiti. yanapatikana katika sura hii.