Browsing by Author "KEFA, NYAIGOTI PATRICK"
Now showing 1 - 1 of 1
- Results Per Page
- Sort Options
Item MATOKEO YA MATUMIZI YA UREJELEZI KATIKA MAHUSIANO KATI YA JAMII YA ABAGUSII NA KIPSIGIS(EGERTON UNIVERSITY, 2024-10) KEFA, NYAIGOTI PATRICKUtafiti huu ulichunguza matokeo ya matumizi yaurejelezi katika mahusiano kati ya jamii ya Abagusii na Kipsigis. Jamii hizi zimekuwa na matumizi ya urejelezi ambayo wanaisimu hawajaifanya tafiti na kuitathmini. Utafiti huu uliongozwa na madhumuni yafuatayo: Kubainisha na kueleza lugha urejelezi inayotumiwa na jamii ya Abagusii na Kipsigis;Kujadili lugha rejelezi inayotumiwa na jamii ya Abagusii na Kipsigis na athari zake katika mahusiano yao na kutathmini mbinu za suluhu zinazotumiwa na Abagusii na Kipsigis kuunda uhusiano bora kati yao. Utafiti huu uliongozwa nandharia ya Utambulisho wa Lugha za Kikabila inayohusu makabila/mbariza binadamu na mahusiano kati ya jamii, yaani (‘Ethnolinguistics identity Theory’ (ELIT). Utafiti huu ni wa kithamano mkabala wa mfano (case study) na ulifanyika katika maeneo ya Borabu na Sotik ambapo ni mpaka ya jamii hizi mbili. Sampuli lengwa ilikuwa ya kimakusudi na ilihusu wazee wanaume 10 na kina mama 10 wenye umri wa miaka 60 na zaidi, kutoka jamii ya Abagusii na Kipsigis na vijana 20 wenye miaka 24 hadi 35 kutoka pande zote za Abagusii na Kipsigis wanaoishi eneo la Borabu – Sotik, kata ya Gelegele tarafa ya Ndanai na kata ya Esise tarafa ya Borabu, eneo hili ni mpaka wa jamii ya Abagusii na Kipsigis. Kwa jumla watafitiwa 60, watfitiwa 30 kutoka jamii ya Abagusii na watafiwa 30 kutoka jamii ya Kipsigis. Mtafiti alishiriki katika mazungumzo katika ukusanyaji wa deta na kisha kufanya unukuzi wa yaliyojiri. Deta ilichanganuliwa na kuwasilishwa kwa njia ya maelezo.Mtafiti alingundua kwamba lugha ya urejelezi huzua rabsha, vurugu na vita. Hivyo basi, wanaobuni sera hawana budi kushirikisha lugha ya urejelezi katika uundaji wa sera zao kuhusu matumizi ya lugha rejelezi ili kusuluhisha mitafaruku inayotokana na jamii zinazopakana. Utafiti huu utafaidi katika kuleta suluhu, amani na utengamano miongoni mwa jamii mbalimbali ulimwenguni, Afrika na Kenya. Utafiti huu utaelimisha jamii, hasa, asasi za serikali na wasimamizi wa kaunti, halmashauri ya kutatua ugonvi miongoni mwa jamii kitaifa, pamoja na kutoa kumbukumbu ambazo serikali kuu na kaunti zinaweza kutumia ili kuleta suluhu miongoni mwa jamii wakati wa mitafaruku. Aidha, matokeo yametoa kumbukumbu za marejeleo ambazo wasomi watatumia ili kufanya tafiti nyingine kati ya jamii mbalimbali kwani matumizi ya urejelezi huzua mitafaruku, rabsha na vita miongoni mwa jamii.