Browsing by Author "Owino, Agull Nicholas"
Now showing 1 - 2 of 2
- Results Per Page
- Sort Options
Item Mifanyiko ya Kimofofonolojia ya Ukuzaji na Udunishaji Nomino za Kiwanga, Kakamega, Kenya(Egerton University, 2016-11) Owino, Agull NicholasMost of Kiwanga nouns transform their internal structures to external structures when augmentated or diminutated. These changes are as a result of morhophonological processes unfolded by {ku-/mi-} nd {xa-/ru-} morphemes interaction with the noun stems. Purposely, this research work intended to describe changes in Kiwanga noun structures under the topic; Morphophonological processes of augmentative and diminutive Kiwanga nouns. The research work objectively endeavored to establish the existence of augmentative and dimunitive morphs. The other objective was to identify different morphophonological processes involved in noun structre transformation and the phonological rules that govern the transformation of the individual nouns from internal to external structures. Phonological Optimal theory provided the basis of the theoretical framework for data analysis. This theory is guided by its three features that describe the stages of noun structure transformation. A total of sixty five nouns formed the research data. The data was collected out of topical discussions on Environment, Wildlife, Domestic animals, Tourism, Body parts, Agriculture etc. A total of thirteen groups comprising of ten participants produced one hundred and thirty nouns ten from each group. From special group discussions and focus group interviews nouns with predetermined phonological features were of concern. Nouns that exhibited similar phonological features were dropped and keeping five nouns in each group making a total of sixty five for analysis and presentation. The research findings justified the research questions that indeed there exists correlation between dissimilar morphemic constituents and the noun stems governed by phonological rules that are a typical linguistic characteristic of Kiwanga nouns. The findings of this research will undoubtedly put Kiwanga on the reference map for future comparative linguistic on Bantu language researches. The research sample was Matungu Sub-county in Kakamega County, Kenya.Item Mifanyiko ya Kimofofonolojia ya Ukuzaji na Udunishaji Nomino za Kiwanga, Kakamega, Kenya(Egerton University, 2016-11) Owino, Agull NicholasBaadhi ya nomino za Kiwanga hubadili maumbo kutoka umbo-ndani hadi umbo-nje inapokuzwa au kudunishwa. Mabadiliko haya husababishwa na mifanyiko ya kimofofonolojia kutokana na uamilifu wa mofu {ku-/mi-} au {xa-/ru-}. Mifanyiko hii hudhihirika mofu za ukuzaji na udunishaji zinapoathiriana na segementi za mizizi ya nomino. Tasnifu ya utafiti huu ilijengwa kwa mada; Mifanyiko ya kimofofonolojia ya ukuzaji na udunishaji nomino za Kiwanga. Lengo la utafiti huu ulikuwa kuonyesha hatua za ukokotezwaji wa maumbo-ndani hadi maumbo-nje ya nomino. Hatua hizi zilibainishwa kwa mofu maalum kuathiriana na segmenti za mizizi, mifanyiko ya kimofofonolojia kukokotoa mabadiliko ya maumbo ya nomino husika na kanuni za kifonolojia kuongoza mifanyiko husika. Mabadiliko ya maumbo ya nomino yalifasiriwa kwa kuongozwa na mihimili ya nadharia ya Fonolojia Umbo-upeo. Mihimili hii ni pamoja na; kihimili cha uzalishi, masharti-zuizi na tathmini. Deta ya utafiti huu ilikuwa nomino sitini na tano za Kiwanga. Nomino hizi zilitokana na mijadala na mahojiano ya kimakundi kuhusu mada kama vile; Kilimo, Ufugaji, Vifaa vya matumizi ya nyumbani, Mazingira, Utalii, Sehemu za mwili nk. Makundi kumi na matatu ya washiriki kumi kumi yalifanya mazungungumzo ya kawaida ili kutaja nomino kumi kwa kila kikundi. Takribani nomino mia moja na thelathini zilichanganuliwa huku nomino zenye sifa maalum za kifonolojia zikizingatiwa. Nyingi zilikuwa na mshabaha wa sifa za kifonolojia na hivyo kuchujwa na kusalia na idadi ya nomino sitini na tano. Deta hiyo iliwasilisha nomino tofauti tofauti zenye sifa maalum za kifonolojia kwa ajili ya uchanganuzi ili kujibu maswali ya utafiti. Matokeo ya utafiti huu yanatarajiwa kukitambulisha Kiwanga kama lugha ya kurejelewa na wanaisimu-linganishi wanapotafitia mifanyiko ya kimofofonolojia katika lugha za Kibantu. Utafiti huu uliendeshwa katika Jimbo dogo la Matungu iliyoko Jimbo la Kakamega nchini Kenya.