SHUJAAZ KAMA KAZI YA FASIHI YA KISWAHILI
No Thumbnail Available
Date
2026-03
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Egerton University
Abstract
Fasihi andishi hushirikisha sio tu fasihi inayowasilishwa kwa njia ya maandishi bali pia fasihi ni
sanaa inayotumia picha na michoro kuwasilisha ujumbe hasa pale picha na michoro hiyo
inaambatanishwa na maneno yaliyoandikwa. Shujaaz ni toleo la katuni ambalo huchapishwa
mara moja kila mwezi na kampuni ya Well Told Story na husambazwa na Gazeti la Saturday
Nation kila Jumamosi ya kwanza ya kila mwezi. Shujaaz ni tofauti na fasihi andishi
tuliyoizoewa katika kazi za kifasihi kwani Shujaaz ni fasihi ya kifani ya kipekee ambayo
inatumia vyote maandishi, michoro, picha halisi, taarifa kuwasilisha tajiriba na ujumbe kwa
jamii husika kama ilivyo fasihi yoyote ili. Hali hii ndiyo iliyozua ari ya utafiti huu. Madhumuni
makuu ya utafiti huu ni kuthibitisha kuwa Shujaaz ni kazi ya fasihi ya Kiswahili ambayo
inahusisha picha za watu halisi, michoro na teknolojia katika uwasilishaji wa ujumbe. Kuafikia
lengo hili, utafiti huu umeweza: kutambua sifa bainifu za Shujaaz kama kazi ya fasihi ya
Kiswahili, kuhakiki Shujaaz kama kazi ya fasihi kwa kutumia vigezo vya uhakiki wa fasihi, na
kutathmini upekee wa Shujaaz kama kazi ya fasihi ya Kiswahili. Nadharia iliyoongoza utafiti
huu ni nadharia ya Metausasa yake Robin na Timotheus (2016) Utafiti huu ni wa kithamano na
data imekusanywa kutoka kwa 10% ya matoleo yaliyochaguliwa kimakusudi miongoni mwa
matoleo 130 yaliyopo ya Shujaaz kufikia mwezi ya Januari 2021. Uchanganuzi wa data
ulifanywa kwa ufasiri data iliyokusanywa kwa mwongozo wa mihimili mahsusi ya nadharia ya
Metausasa. Matokeo ya utafiti yamewasilishwa kwa njia ya maelezo. Matokeo haya
yanatarajiwa yataweka wazi kuwa Shujaaz ni kazi ya fasihi na yafaa kuthaminiwa, kusomwa na
kuhakikiwa kama tanzu nyinginezo za fasihi. Kazi hii inatarajiwa kuwa mwongozo wa kutafitia
kazi nyinginezo zinazofanana na kazi ya Shujaaz.