KIARIE, MBURU CHARLES2026-06-302026-06-302026-03http://41.89.96.81:4000/handle/123456789/3873Fasihi andishi hushirikisha sio tu fasihi inayowasilishwa kwa njia ya maandishi bali pia fasihi ni sanaa inayotumia picha na michoro kuwasilisha ujumbe hasa pale picha na michoro hiyo inaambatanishwa na maneno yaliyoandikwa. Shujaaz ni toleo la katuni ambalo huchapishwa mara moja kila mwezi na kampuni ya Well Told Story na husambazwa na Gazeti la Saturday Nation kila Jumamosi ya kwanza ya kila mwezi. Shujaaz ni tofauti na fasihi andishi tuliyoizoewa katika kazi za kifasihi kwani Shujaaz ni fasihi ya kifani ya kipekee ambayo inatumia vyote maandishi, michoro, picha halisi, taarifa kuwasilisha tajiriba na ujumbe kwa jamii husika kama ilivyo fasihi yoyote ili. Hali hii ndiyo iliyozua ari ya utafiti huu. Madhumuni makuu ya utafiti huu ni kuthibitisha kuwa Shujaaz ni kazi ya fasihi ya Kiswahili ambayo inahusisha picha za watu halisi, michoro na teknolojia katika uwasilishaji wa ujumbe. Kuafikia lengo hili, utafiti huu umeweza: kutambua sifa bainifu za Shujaaz kama kazi ya fasihi ya Kiswahili, kuhakiki Shujaaz kama kazi ya fasihi kwa kutumia vigezo vya uhakiki wa fasihi, na kutathmini upekee wa Shujaaz kama kazi ya fasihi ya Kiswahili. Nadharia iliyoongoza utafiti huu ni nadharia ya Metausasa yake Robin na Timotheus (2016) Utafiti huu ni wa kithamano na data imekusanywa kutoka kwa 10% ya matoleo yaliyochaguliwa kimakusudi miongoni mwa matoleo 130 yaliyopo ya Shujaaz kufikia mwezi ya Januari 2021. Uchanganuzi wa data ulifanywa kwa ufasiri data iliyokusanywa kwa mwongozo wa mihimili mahsusi ya nadharia ya Metausasa. Matokeo ya utafiti yamewasilishwa kwa njia ya maelezo. Matokeo haya yanatarajiwa yataweka wazi kuwa Shujaaz ni kazi ya fasihi na yafaa kuthaminiwa, kusomwa na kuhakikiwa kama tanzu nyinginezo za fasihi. Kazi hii inatarajiwa kuwa mwongozo wa kutafitia kazi nyinginezo zinazofanana na kazi ya Shujaaz.SHUJAAZ KAMA KAZI YA FASIHI YA KISWAHILIThesis