Abstract:
Tasnifu hii imejishughulisha na suala la hadithi katikajamii ya Waigembe, na hasa ikizingatia nafasi ya hadithi hizo katika ujamiishaji. Hadithi zimedhihirisha kuwa na uhusiano wa karibu na utamaduni na mazingira yajamii husika. Vile vile, imedhihirika kuwa hadithi huwa na majukumu maalum na muhimu ya kutekeleza katika jamii. Katika sura ya kwanza, msingi ambamo tasnifu hii imcjengcka unabainika. Baadhi ya mambo muhimu ambayo yameshughulikiwa katika sura ya kwanza ni pamoja na somo la utafiti, madhumuni na sababu za kuichagua mada, upco wa tasnifu, mbinu za utafiti, na nadharia ambayo imetumika kuzichambua hadithi katika tasnifu hii. Katika sura ya pili, maandishi kuhusu hadithi kama utanzu wa fasihi simulizi yamcshughulikiwa. Kuna waandishi wengi sana ambao wameushughulikia utanzu wa hadithi. Baadhi yao wameuangalia utanzu huu katikajamii mahususi, na wenginc wameushughulikia kwa kijumla tu bila kurejelea jamii mahususi. Katika kuchunguza maandishi ya wataalam mbalimbali kuhusu hadithi, wasomi wa Kiafrika wameshughulikiwa kwa upana zaidi. Sura ya tatu ndiyo sura muhimu zaidi katika tasnifu hii. Uchambuzi wa hadithi mbali mbali umedhihirisha kuwa hadithi hutekcleza majukumu maalum katika uelimishaji na ujamiishaji wa wanajamii wa umri na hadhi mbalimbali miongoni mwa Waigembe. Utanzu wa hadithi umcdhihirika kwamba hulekeleza wajibu mkubwa wa mawasiliano. Kuhusu mbinu za utambaji, ni dhahiri kuwa zinachangia pakubwa uelcwekaji wa ujumbe unaopitishwa kwa njia ya utambaji Mbinu zilizoshughulikiwa katika sura hii ni pamoja na utcndaji, uchaguzi wa maneno, nyimbo, takiriri, nu tanakali-sauti. Utambaji wa hadithi umejitokeza kama sanaa inayowasaidia watoto kuwa wabunifu na kuwa na ujasiri. Waaidha, wanapopewa nafasi ya kutamba hadithi katika vikao vya utambaji, watoto wanapala uzoefu wa kuzungumza hadharani. Katika sura ya nnc, uchambuzi wa hadithi umefanywa kwa undani zaidi kwa kuoanisha mambo yanayojitokeza katika hadithi na yale yanayopatikana katika utamaduni wa jamii iliyozilunga hadithi zenycwe. Imedhihirika kuwa hadithi ni zao la utamaduni wajamii iliyozitunga na, vilcvile, ni sehemu ya utamaduni hu0_ Kwa hivyo hadithi, kama zao la ulamaduni na sehcmu ya utamaduni, huwa zinawaelimisha wanajamii kuhusu mambo muhimu yanayopaswa kuzingatiwa katika jamii. Katika sehemu hii pia, mtafiti amejaribu kuonyesha kuwa hadithi hazikuwa muhimu tu katika zama za mababu zetu, bali ni muhimu hata katika jamii zctu leo. Kwajinsi hii basi, mafunzo yanayopatikana katika hadithi hayajapitwa na wakati.Katika sehemu ya pili ya sura hii, miktadha ya kijamii ambamo hadithi hutambwa imeshughulikiwa, na imcbainika kuwa miktadha hii huwa inachangia uelewekaji wa ujumbe katika hadithi. Kwa jumla, tasnifu hii imejaribu kuonyesha kuwa hadithi ni utanzu ulio na umuhimu mkubwa sana katikajamii, na hautumiwi kuwaelimisha na kuwaburudisha watoto tu, bali unatumiwa na kila mwanajamii.