DSpace Repository

Kung za kiundishi za kimajaribio katika riwaya teule za kisasa za Kyallo Wadi Wamitila

Show simple item record

dc.contributor.author Mwikali, Janice Mutua
dc.date.issued 2023-06
dc.date.accessioned 2023-12-13T12:09:50Z
dc.date.available 2023-12-13T12:09:50Z
dc.identifier.uri http://41.89.96.81:8080/xmlui/handle/123456789/3045
dc.description.abstract Riwaya za kimajaribio ni kazi andishi za kibunifu zilizoandikwa kwa kufuata mitindo mipya ya uandishi Wa riwaya za kisasa ambapo mbinu zinazotumiwa hukiuka uhalisia Wa kihistoria Wa kijadi hasa katika uwasilishaji wa vitushi. Kwa kuwa wasanii wana uhuru wa kuandika jinsi Wapendavyo, matumizi ya mbinu za majaribio yamepelekea kuibuka kwa riwaya mpya ya Kiswahili inayoegemca mkondo wa “uhalisia-mpya.” Wamitila ni mmojawapo wa waandishi wa riwaya za Kiswahili anayetumia mbinu za kimajaribio kama kunga ya uandishi Wa bunilizi zake za kisasa. Kiini cha utafiti huu kilikuwa kubainisha namna mwandishi anavyozitumia mbinu za kimajaribio kama msingi mkuu Wa ubunifu katika riwaya anazozibuni. Vilevile, utafiti huu uliazimia kubainisha mbinu mahususi anazotumia Wamitila kuangazia maswala yanayoibuka katika jamii. Kuafikia haya, riwaya tatu za mwandishi zimeteuliwa kimaksudi. Ni pamoja na: Musaleo, Msichamz wa Mbalamwezi na Mwandishi, Msomaji na Mchapishaji. Mtafiti ameweka bayana mbinu za kimajaribio anazotumia Wamitila kwa kuzitambulisha na kufafanua vipengele mbalimbali vya mbinu husika katika riwaya teule. Aidha, utafiti ulichunguza jinsi mbinu hizo zilivyotumika kama kunga ya uandishi na kifaa cha kuwasilishia ujumbe katika riwaya za kisasa. Utafiti uliongozwa na nadharia ya usasaleo kama ilivyoasisiwa Jean-Francois Lyotard, Jean Baudrillard, Jurgen Habermas na Fredric Jameson. Kwa mujibu Wa nadharia ya usasaleo utaratibu maalum wa kijamii uliozoeleka huyumbishwa. Nadharia hii inakiuka matumizi ya riwaya kuu ya kihalisia na kupendekeza kutumika kwa riwaya mpya iliyojawa na uradidi unaoleta maana pana kama njia ya kuelezea maswala muhimu ya jamii. Kwa kuwa data iliyokusanywa ilikuwa ya kithamano, mtafiti alisoma riwaya teule za mwandishi na kudondoa mbinu mbalimbali za kimajaribio zilizotumika katika bunilizi husika. Utafiti ulibaini kuwa Wamitila amewasilisha maswala mahususi yanayohusu jamii kwa kutumia mbinu za kimajaribio kama kunga yake ya ubunifu. Hatimaye, mtafiti alibaini kuwa simulizi fupi, urcjeleomatini, taashira, dayolojia, uhalisiajabu, tamathali za lugha ndivyo vipengele vikuu vya kimajaribio vinavyokatiza usimulizi katika riwaya teule. Utafiti huu umesisitiza kuhusu jinsi waandishi wa riwaya ya kisasa ya Kiswahili Wanavyoyasawiri maswala ya kijamii katika bunilizi zao. Matokeo ya utafiti ni nyongeza kwa taaluma ya ujuzi na ufahamu unaohusu kunga za uandishi wa kazi za fasihi. Aidha, ni mchango katika kuwaelekeza Waandishi na Wasomaji kuhusu uelewa Wa mbinu za kimajaribio kama kunga ya kuwasilisha dhamira na maudhui katika riwaya ya Kiswahili en_US
dc.language.iso en en_US
dc.publisher Egerton University en_US
dc.subject Riwaya Teule en_US
dc.title Kung za kiundishi za kimajaribio katika riwaya teule za kisasa za Kyallo Wadi Wamitila en_US
dc.type Thesis en_US


Files in this item

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search DSpace


Advanced Search

Browse

My Account